Burudani

Nisher na Weusi ni kama familia, fahamu kwanini. Pia azungumzia sababu za baadhi ya video alizotuma Channel O kutopitishwa na kituo hicho

Director wa video kutoka Arusha Nisher ambaye siku zinavyozidi kwenda anazidi kueleweka na Watanzania kwa kile anachokifanya, ameelezea sababu za kwanini baadhi ya video alizotuma katika TV ya kimataifa Channel O ya Afrika Kusini hazikupitishwa.

Nisher

Nisher ambaye kwa siku chache zilizopita toka atoe video ya Nikki Wa Pili, Joh Makini na G-Nako ‘Nje Ya Box’ ameongeza heshima katika game ya Tanzania, kutokana na video hiyo kupokelewa vizuri sana, na hatimaye pia kuweza kupitishwa na kuanza kuchezwa na Channel O.

Akizungumza na Tovuti ya Times Fm, Nisher amesema alituma jumla ya video sita kwa kituo hicho ikiwemo Nje ya Box, lakini kuna baadhi ambazo hazikupitishwa.

“Nilituma kama sita hivi, sema kuna baadhi zilizopita, ila nyingine wakaeleza kwamba hazitachezwa kwa sababu sio kitu ambacho walikuwa wanakitafuta, au sio kitu ambacho wanakiangalia kukirushwa kwenye station yao.” Alisema Nisher

Nisher aliongeza kuwa kati ya nyimbo ambazo hazikupitishwa moja ya sababu ni aina ya muziki, sio kitu walichokuwa wanakihitaji.

“Kwa hiyo zilizopita ndizo zilizokuwa zinakidhi kile wanachokihitaji wao, mojawapo ilikuwa ikiwa ni pamoja na nyimbo..muziki pia, yaani aina ya muziki sio kitu ambacho walikuwa wanakitafuta pia.”

Video zilizotumwa na kupita ni pamoja na ‘Nje Ya Box’ ambayo ndio ilikuwa ya kwanza kuanza kuchezwa Channel O, nyingine ambazo zimepita ni ‘My Baby’ ya Mirror, ‘Kijukuu’ ya Young Dee, na ‘Mama Yeyoo’ ya G-Nako ambazo muda wowote zitaanza kuonekana.
Zile ambazo hazikupitishwa ni pamoja na ‘Nakomaa na Jiji’ ya Shilole na ‘Amani ya Moyo’ ya Feza Kessy.

Upande mwingine Nisher amezungumzia nafasi ya weusi katika mafanikio ya kazi zake kuweza kutambulika na kukubalika Tanzania toka alipoingia rasmi kwenye game.

Hiki ndicho alichokiandika Instagram kuwashukuru Weusi kwa mchango wao katika mafanikio hayo:

“Baba Yangu @joh_makini Kaka zangu @gnakowarawara @nikkwapili bila nyie Nisingekua Hapa Nilipo…Nawapenda Mpaka siku Yangu ya Mwisho…. kazi tulizo zifanya zimekua na NGUVU ZAIDI machoni mwa Watu na habari zake zimekua na SAUTI zaidi masikioni mwa Watu… since SIJUTII, MAMA YEYOO, NJE YA BOX…. kuna ka mwendo hapo… na bado Tunatakiwa Kukalisha zaidiiiiii …. Lets Get it, Tutishe kabisa!!!! 2014… LOVE YOU HOME BOYS WE FAMILY FOREVER!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents