Burudani

Nisher: Hanscana na Khalfan si tishio kwangu, wakifikia views zangu na hela ninayotoza labda tutaongea (Video)

Muongozaji wa video ya XO ya Joh Makini na 13 ya Young Killer, Nisher amedai kuwa waongozaji wapya wanaofanya vizuri kwa sasa, Hanscana na Khalfan si tishio kwake.

Nisher ameiambia Bongo5 kuwa hatua waliyopo sasa ndio ile aliyokuwa nayo miaka miwili iliyopita wakati akitafuta nafasi kama muongozaji wa video.

Khalfan aliwahi kuwa msaidizi wa Nisher na alipoondoka wawili hao waliingia kwenye vita vya maneno kwenye mitandao ya kijamii huku Hanscana pia akishiriki kumjibia Khalfan ambaye hufanya naye kazi pamoja.

“Mimi kiukweli ninawatakia kila lakheri, mimi sina kinyongo wala ubaya na wao nadhani waendelee, wakazane watu ndio wataamua,” amesema Nisher.

“Mimi kazi zao hazinitishi kwasababu catalogue yangu ndefu inaeleweka, issue tunayoangalia ni numbers. Ninaposema tunaangalia numbers tunaangalia vitu kama views, fan base, status, tunaangalia money – how much money are they making! Tunaangalia video yangu moja ni shilingi ngapi na video yako moja ni shilling ngapi, tuanze kuongea kuanzia hapo.”

“Ukishaweza kunifunika hapo nadhani tunaweza tukaongea sasa kwasababu tunakuwa equal. Lakini sidhani kama wanaweza wakajinadi kwamba wamefika, bado. Mimi mwenyewe bado sijafika nakazana, kuna mahali napataka sijapapata. So na wao wanapodhani kuwa wanakuwa wamenifikia wanakuwa wanakosea, lakini wakibaki na njaa kwamba tunataka tufike level kubwa watafika mbali.”

Tazama video hiyo hapo juu kumsikia zaidi (amewaongelea Hanscana na Khalfan kuanzia 14:28).

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents