Burudani

Nisher: Game linanoga sasa hivi, ushindani wa video za muziki ni mkubwa

Muongozaji wa video nchini, Nisher amesema waongozaji wengi wa video nchini wanazidi kuboresha kazi zao na ushindani ni mkubwa.

06 - insta 2

Nisher amesema kama kila muongozaji akiendelea kujituma na kuwa mbunifu zaidi, wasanii wanaokimbilia Kenya kushoot video wanaweza kubadilisha mawazo na kuzifanya video zao hapa hapa.

“Directors wengi wa Bongo wamejitahidi sana kufanya kazi nzuri kwa wasanii wao,” Nisher ameiambia Bongo5. “Sasa hivi kiukweli game linanoga kwasababu hata unafanya kazi unaona kuna competition fulani inaendelea ambayo ni positive tofauti na miaka ya hapa nyuma kidogo.”

nisher
Mwaka huu Nisher alishinda tuzo ya muongozaji wa video za muziki zinazopendwa kwenye Tuzo za Watu

Amesema ushindani huo umetokana na waongozaji wote kufuatilia kazi za wengine na kwakuwa wengi wanafanya vizuri, kila mmoja anataka kufanya kazi nzuri zaidi.

“Hiyo inawafanya watu wanakuwa creative, wanaumiza vichwa. Sasa hivi hata ukiangalia kwenye TV unaona usafi,” ameongeza Nisher ambaye hivi karibuni aliongoza na kutayarisha video ya wimbo wa Young Killer aliomshirikisha Fid Q ‘13’.

Nisher amesema kutokana na kuanza kuhusisha timu kubwa na vifaa vingi zaidi, hata bei ya kufanya video imepanda. “Mwaka huu bei zimekuja juu kidogo na standard imekuja juu hata ya production. Utaona sasa hivi tuna malori ya taa, malori ya cranes, yanabeba vitu mbalimbali, kuna crew kubwa. Vitu kama hivyo wasanii ndio wanapenda, wakiona wanasema ‘dah hapa kweli tunashoot video, sio ile unatoa tu mtaani na kikamera.”

Pamoja na kudai kuwa gharama za video hutokana na makubaliano baina yake na msanii, kiwango anachotoza sasa ni kuanzia shilingi milioni tano na mwakani anatarajia kupandisha akidai kuwa ni kutokana na kupanda kwa gharama ya vitu mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents