Habari

Nisher awajibu waliomkosoa juu ya video mpya, ‘angalia na hadhi ya nyimbo inayostahili kufanyiwa kichupa’

Jumapili iliyopita director Nisher ameachia video mpya ya msanii aitwaye AMA G kutoka Mwanza, ikiwa ni video ya sita kutoa toka mwaka huu umeanza. Baadhi ya mashabiki wa kazi zake wamepongeza kwa kuendelea kufanya video nzuri, lakini baadhi yao wameonekana kutoridhishwa na kiwango cha msanii aliyemfanyia video hiyo.

Nisher

Haya ni majibu ya Nisher kwa wale waliomkosoa kuhusu msanii aliyemfanyia video:

“Ok Seriously this has to Stop! Kwanza Ieleweke kabisa Kua saivi mimi nipo Very Expensive Kufanya Videos TZ… Nakama Hamja Shtukia nimepunguza kasi yakutoa Kazi Mpya, Kwanini? Watu Hawataki kutoa hela!!! Hiyo sio changamoto kwangu, ni changamoto ya Wasanii…

Kitendo cha Huyu Kijana Ku-WEZA kunilipa kufanya Music Video Yake shilingi MILIONI 5 CASH na Kuja Onset na Pamba zake tu, Kwahilo NAMSIFU SANA!!! Bado aliniambia alitumia milioni moja zaidi kwaajili ya Kusafiri kutoka Mwanza Kuja Arusha, na kulipia hotel yake pamoja na Kuandaa mavazi Nilio Mtajia pamoja na Kulipa extra cost Zote! Namsifu sana…

Pili ieleweke kua Huyu bado ni Msanii mchanga, Alichoniomba Nikwamba Nimasaidie tu Kupata Jina Langu (NISHER) kwenye kazi yake… Na aliniambia kabisa Kwamba anajua yeye bado mchanga ila aliniomba Sana kwa moyo wote akasema Yupotayari Kunilipia Gharama zozote zile ili tu Apate Jina Langu kwenye Kazi yake!!! Huyukijana Anatakiwa Apigiwe makofi… Tena amewaaibisha watu wote wenye nyimbo nzuri walioshindwa kunilipa… You should be ASHAMED OF YOURSELVES KWA KUMPONDEA HUYU KIJANA!!!!!!!!!!!!!!!! Nimemaliza.”

Hizi ni baadhi ya comments kuhusu video hiyo:

tonyjom-nilimsikia director kelvin Bosco akisema hua anasikiliza nyimbo za wasanii km Ni mbya anakataa kufanya nao kaz coz wanashusha CV yako,its beta ukaiga Hilo.

allenizo168-Video nzuri msanii kazingua baab angalia na hadhi ya nyimbo inastaili kufanyiwa kichupa na director nisher manake haelewiki huyo artist vocal hana mashaili mabovu

verbsmedia-Dis vid imebidi niichek bila sauti,…napenda sana kazi zako @nisherbybee ,bt zngatia wasanii unaofanya nao kazi,huyu hakua mzuri!


rahim chardluck-nyimbo yak underground sana..japo video nzuri….

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents