Burudani

Nisher adai wasanii wanawadharau madirector wa bongo na kwenda kushoot nje, asema video ya ‘Unanichora’ pekee ndio aliyolipwa hela nyingi M10

Ikiwa ni jana (July 23) tu mwimbaji wa ‘Ndagushima’ Ommy Dimpoz alitoa wito kwa wadau kuwekeza kwenye vifaa vya kutengenezea video ili wasanii wa bongo wasilazimike kwenda nje kutengeneza video zao kwa gharama kubwa, mshindi wa Tuzo za Watu 2014 director Nisher amewatumia lawama baadhi ya wasanii wakubwa kwa kuwadharau madirector wa ndani na kuwaona hawajui.

Nisher TZW

“Mi sipati logic wasanii wanavyosema wanaweza kulipa sijui milioni za hela wapi…mi napigiwa simu na wasanii wakubwa lakini kila anaekupigia anasema mi sina hela lakini mi naweza kukugharamia chochote unachotaka tushoot video.” Amesema Nisher kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.

Nisher ambaye ana takribani miaka miwili toka aanze kutengeneza video amesema amekua akipokea simu za wasanii wakubwa wanaotaka kufanya nae video lakini wote huwa wagumu kutoa bajeti nzuri kwaajili ya video. Ameongeza kuwa video mpya ya Ben Pol pekee ndio aliyolipwa pesa nyngi.

“Unaanzaje na kauli halafu na wakati mi nasoma kwenye Internet kwamba umelipa sijui kiasi gani gani gani kwenye video flani flani, nafikiri video ya Ben Pol juzi tu ambayo tuliifanya ‘Unanichora’ labda ndio video niliyopata hela nyingi kwa kiasi flani kwa sababu video iligharimu karibu milioni 10 hivi. Mi nadhani tunachukuliana poa na kudhariana kiukweli. “

Nisher ambaye makazi yake ni Arusha amesema vifaa vya kukodi vinapatikana Dar isipokuwa vina gharama kubwa na ndio sababu msanii anapomlipa vizuri director anauhakika wa kufanyiwa kazi nzuri na kusambaziwa hata TV za nje pia.

“Kwa Mfano ukinilipa milioni 5 au 10, una uhakika kwamba hela hiyo hiyo itatumika kusambaza kazi yako[…] kufanya kila kitu. Vyombo vipo cranes nini, cranes zenyewe za kukodi kwa siku laki 5, camera zipo za kukodi Red Camera unaambiwa labda dola 800 kwa siku, nani atakupa hiyo hela? Hivi vitu vinakatisha tamaa wasanii hawatukubali wanatuona kama hatujui.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents