Burudani

Nisha asema amekaa kimya bila kutoa filamu kutokana na maoni ya mashabiki

Mkali ya filamu ya ‘Pusi na Paku’, Salma Jabu aka Nisha amesema kuwa maoni ya mashabiki wa filamu zake yalimfanya akae kimya toka mwaka uanze mpaka sasa.

Nisha akiwa katika picha ya utengenezaji wa filamu yake mpya ya  Zena na Betina

Nisha ameiambia bongo5 kuwa alipokea maoni mengi kuhusu aina ya uigizaji wake hali iliyomfanya asitoe kazi mpaka ajipange kwanza.

“Unajua nilifanya kazi nyingi sana mwaka jana na nimepokea maoni mengi, hasa hasa watu wananitaka nibadilike kidogo katika jinsi ninavyochekesha, kwahiyo mimi na kampuni yangu tukakaa chini na kuyafanyia kazi maoni yao, kwahiyo mwaka huu bado sijatoa filamu mpaka sasa kwaajili ya kufanyia marekebisho katika baadhi ya mambo na baada ya hapo soon utaanza kuona kazi mpya,” alisema Nisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents