Bongo Movie

Nisha adai filamu zake zinaongoza kwa mauzo sokoni

Msanii wa filamu za vichekesho anayetamba na filamu ya Tikisa,Gumzo na Pusi na Paku, Nisha Jabu amesema amekuwa akipokea takwimu za mauzo mazuri ya filamu zake ambazo zinaonyesha ndio zinauza zaidi sokoni kwa sasa.

1554478_718817938141387_704073968_n

Nisha ameiambia Bongo5 kuwa wasambazaji wa filamu hizo wamemuambia amefikia kiwango kikubwa zaidi cha mauzo sokoni.

“Namshukuru mwenyezi Mungu kila kazi ambayo natoa Nishas film Production inafanya vizuri na zinakuwa gumzo yaani. Kila mtu anaitazama na kuhusu masuala ya soko Alhamdulillah zinafanya vizuri,” amesema. “Ukiwa mfanyabiashara lazima uwe unakiangalia unachokitoa,yaani watu wanakipokokea vipi? Kwanza kabisa naambiwa na wamachinga wanaouza DVD hizi, je? katika filamu hii na hii ipi imefanya vizuri wananijibu, kingine mashabiki zangu wanaitana majina ninayotumia kwenye filamu mbalimbali. Hii ni dalili nzuri kwamba anakifuatilia ninachokifanya. Kingine kikubwa zaidi ni kutoka kwa watu ambao nawauziA kazi, kama una kazi yako inafanya vizuri ndio wanakupa kipaumbele. Yaani ndio bongo iko hivyo. Hufanyi vizuri huwezi kupewa kipaumbele. Kwahiyo wananipa support pia kuna kitu kinakuwa kinaitwa marks za mauzo kwamba kuna movie nyingine zinaweza zikatoka leo mpaka mwezi hazijafikisha asilimia mia moja,lakini mimi karibia movie zote ambazo nimezitoa hazijafikisha siku tatu zimeshavuka asilimia mia moja. Yaani hapo maana yake kama watu wanatoa copy mia sita,basi movie zangu zinatoa kopi elfu mbili kwenda mbele. Kwahiyo inanionyesha fika kwamba kazi zangu zinafanya vizuri. Kingine naona mashabiki zangu mitaani jinsi gani wanaipokea, jinsi gani wananichukulia. muonekano wangu wa mwaka 2012,2013 sio kama mwonekano wangu wa 2014, yaani naona kabisa mashabiki wangu wananipokea vipi.”

Nisha amesema matarajio yake ni kuendelea kufanya vizuri zaidi hadi kufanikiwa kimataifa.

“Kikubwa kila siku ni kubuni vitu vipya ambavyo havijawaHi fanyika na kusonga mbele zaidi,” amesema Nisha. “Matarajio pia ya msanii ni kufanya kazi nje, kimataifa zaidi ila hata mbuyu ulianza kama mchicha,kidogo kidogo hivyo hivyo tutafika. Kwahiyo kikubwa tunajifunza zaidi, tunabuni kitu gani ambacho tulikosea mwanzo ili sasa hivi tufanye vizuri zaidi, kufanya kazi kwa bidii,kutokujibweteka na kulewa sifa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents