Burudani

‘Niombeeni’ – asema Chidi Benz, kupanda kizimbani leo

Rapper Rashid Makwiro aka Chid Benz anapanda kizimbani Jumanne hii, November 11 kwenye mahakama ya hakimu mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam.

Chid Beenz_full

Rapper huyo ambaye yupo nje kwa dhamana kufuatia kukamatwa na madawa ya kulevya hivi karibuni, amewaomba mashabiki wamwombee.

“Kesho napanda mahakamani asubuhi pale kwa hakimu mkazi kissutu..niombeeni kheri koz najua wapo wanaonihitaji bado.#vitu mbali mbali,” aliandika Chidi Benz kwenye Twitter.

Chid Benz’ alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroine na bangi tarehe 24 October akiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akijiaanda kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye show.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents