BurudaniDiamond Platnumz

Ninaipenda Tanzania daima – Davido

Kwa Davido, Tanzania itaendelea kukaa katika nafasi muhimu sana moyoni mwake. Katika wakati ambao wengi tunadhani ameisahau, hitmaker huyo wa How Long, ameibuka na kuthibitisha kuwa bado ana mapenzi tele na ya milele kwa nchi ya Magufuli.

15056647_190729444667106_3553966230622699520_n

Ameufungua moyo wake kwenye post ya Diamond katika mtandao wa Instagram ya show yake ya mjini Harare nchini Zimbabwe – Watora Mari iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Kwenye post hiyo ya show hiyo iliyofana na kushuhudia akiujaza ukumbi mkubwa wa HICC akiwa na mwenyeji wake Jah Prayzah, Diamond aliandika:
This Song Called #NumberOneRemix it has more than 18.5 Million Views on Youtube….. Go watch it and enjoy the Mix of Bongo flavour and Naija.”

Post hiyo ilimkuna Davido aliyeandika na kujibiwa na Diamond kama inavyoonekana hapo chini:

davido

Kama ambavyo Jah Prayzah anamshukuru Diamond kwa kumtambulisha kwenye ramani ya muziki wa Afrika, Diamond atamshumkuru milele Davido kwa kumpa shavu kwenye remix ya Number One iliyompa staa huyo wa Tanzania umaarufu mkubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents