Burudani

Nimeshaenda sana kwa waganga lakini sikuona mabadiliko yoyote – Galatone

Msanii Galatone ameweka wazi kuwa alishawahi kwenda kwa wa Waganga wengi wa kienyeji ili afanikiwe kwenye sanaa ya muziki anayoifanya.

samaki-galatone-559x520

Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm ijumaa iliyopita, Galatone amesema ilifika kipindi alichoka katika harakati za kuuhangaikia muziki ndipo ikamlazimu kuingia katika nguvu za giza.

“Nimefanya sana nimeenda kwa Waganga maana kuna kipindi nilichoka kabisa nkasema acha nikajaribu, nshavunja nazi, kuchinja kuku na kila kitu yani ili tu nitoboe kwenye game,” alisema.

Galatone amekiri kuwa hakupata chochote na wala hakuona mabadiliko yoyote ndipo akaamua kuachana na mambo hayo na kumtegemeea Mungu tu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents