Burudani

Nimekasirika na nipo tayari kupanda ndege mwaka huu – Dully Sykes

Dully Sykes amekasirika na yupo tayari kuvunja mwiko wake wa kutopanda ndege mwaka huu.

Dully

Dully ni muoga wa kupanda ndege kwa miaka mingi.

Akiongea na Bongo5, muimbaji huyo amesema ili kukabiliana na ushindani kimuziki, mwaka huu amejiandaa kupanda ndege na kwenda kushoot video Afrika Kusini.

“Nilikuwa muoga wa ndege lakini sasa hivi nipo tayari kupanda,” amesema. “Nafikiria kuvunja mwiko, na tayari nimeshavunja kwasababu naanza kupanda soon. Kwahiyo naanza nataka kwenda kufanya video zangu na Adam Juma South Africa na tayari nimeshapiga moyo konde nasema kwamba nimeamua napanda ndege naenda nchi za nje kufanya kazi yangu,” ameongeza.

“Nafikiri napofanya hivyo, vijana wenyewe wakisikia hii habari nafikiri watakuwa wamepata wasiwasi kwamba kaka amekasirika.”

Hata hivyo Dully amedai kuwa pamoja na kupiga moyo konde kupanda ndege hivi karibuni, bado ni muoga. “Bado naogopa, lakini nitapanda kwasababu mwanasaikolojia ameniambia siku unapanda na siku hiyo hiyo uoga unaisha.”

Woga wa kupanda ndege kwa Dully Sykes unatokana na wasiwasi kuwa ndege inaweza kuanguka.

“Unaweza ukaweka hata hisia chumbani kwako kwamba ukuta utadondoka basi ndio hivyo tu.”

Dully si staa wa kwanza duniani kuogopa kupanda ndege.

Wasanii wengine duniani ni pamoja na Megan Fox, Jennifer Aniston, Sandra Bullock, Ben Affleck, Dennis Bergkamp, Fat Joe na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents