Burudani

Nikki wa Pili: Video ya ‘Gere’ imeupiku ubora wa video ya ‘Nje ya Box’

Rapper Nikki wa Pili wa kampuni ya Weusi amesema changamoto waliyokuwa nayo baada ya kuachia video ya ‘Nje ya Box’ ni kutengeneza video inayofuata itakayokuwa kali zaidi kuliko hiyo.. na hilo wamefanikiwa kulifanya kwa kushoot video ya ‘Gere’ nchini Kenya.

AMVCA-Trophy-
Mmoja wa wasichana watakaonekana kwenye video hiyo

“Gere tumeshafanya na imeipiku ‘Nje ya Box’ katika misingi ya creativity, quality na namna picha inavyoonekana,” Nikki wa Pili ameiambia Power Jams ya East Africa Radi. “Halafu pia tumekuja na taste mpya unajua Nisher ni bora ana taste yake na Inos ni bora ana taste yake, ukiangalia video ya Jaguar, Octopizzo. Kwahiyo tumefanya video kali sana. Tunategemea impact itakuwa kubwa kwasababu video ni kali.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents