Burudani

Nikki Wa Pili: Nguvu ya muziki wa nyumbani bado imeonekana ni kubwa zaidi ya muziki wa kigeni

Msemaji wa kundi la Weusi Nickson Simon a.k.a Nikki Wa Pili ni miongoni mwa wasanii waliopanda kwenye jukwaa la Fiesta 2014 kwenye viwanja vya Leaders, Dar Jumamosi October 18 akiwa na Joh Makini, Lord Eyez na G-Nako.

Nikki wa Pili

Nikki ambaye pia hakupitwa na show za wasanii wengine alikuwa na machache ya kusema kwa kile alichokiona kwenye show hizo kuhusiana na muziki na wasanii wa Bongo.

“Nguvu ya muziki wa nyumbani bado imeonekana kwamba ni kubwa zaidi ya muziki wa kigeni kwasababu tumeona wasanii wa nyumbani wamepokelewa kwa nguvu sana hata kulikoni baadhi ya wasanii wa kigeni waliokuja.” Nikki ameiambia BONGO 5 leo.

“Na pia namna ya ushiriki wa wa performance kati ya msanii wa nyumbani na mafans ulikua ni mkubwa kulikoni wasanii wa kigeni na mafans kwahiyo naamini mafans wengi pale walikuwepo kwaajili ya wasanii wa nyumbani kwa kuangalia ule ushirikishi hata Joh Makini wakati anaperform kiwango gani mashabiki wanashiriki kwenye ile performance na Joh Makini….”

Rapper huyo wa ‘Sitaki Kazi’ ametoa ushauri kwa wasanii wa Bongo kutokana na mapungufu aliyoyaona kwenye tamasha hilo.

“Kuna wasanii bado wanatatizo la kwenda live… kwakweli ina distort kwakweli cd ikiwa inaimba na wewe unaimba show haiwi kali, kwahiyo wangeweka nguvu kwenye kuimprove performance kwasababu performance ndio bidhaa ndio kile ambacho tunawauzia mashabiki ndio bidhaa ya mwisho kwahiyo ukiharibu performance umeshaharibu soko lako kwasbabu watu wanakuja kwenye show wanakuja kuinunua ile bidhaakwahiyo ile bidhaa inabidi iwe na ubora wa hali ya juu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents