Bongo5 MakalaBurudani

Nikki wa Pili aelezea mambo ‘Interesting’ yaliyojitokeza wakati wa kushoot ‘Nje Ya Box’

Video ya Nikki wa Pili, Joh Makini na G-Nako ‘Nje Ya Box’ ndio imekuwa talk of the town toka ilipoachwa rasmi mwishoni mwa wiki iliyopita January 24.

Unapoitazama video sio rahisi kufahamu vitu vya nyuma ya camera ambavyo vilijitokeza wakati wa process nzima ya toka inaanza kutengenezwa.

Nikki wa Pili amezungumza na Bongo 5 na kuelezea baadhi ya vitu ‘Interesting’ vya behind the scene vilivyojitokeza wakati wa utengenezwaji wa video hiyo, au ambavyo vimehusika.

1.Intro ya Video

Ile sehemu ya intro ya video ambapo Nikki anaonekana amekaa sehemu na baadaye kusinzia, ilitumia siku nzima kushoot yenyewe tu.
“Ile sehemu ya intro mpaka tuligombana na Nisher, maana tulishoot siku nzima hiyo part pake yake, kwasababu mimi nilikuwa nimeigiza mpaka nikawa nimechoka yani sababu naona dah mbona navyopiga sipatii, vingine naona nafanya vizuri lakini anasema rudia, lakini mpaka tunagombana Nisher alikuwa amshapata ambacho alikuwa anahitaji.”-Nikki

2. Video Vixen

Model anayeonekana katika video ya ‘Nje Ya Box’ hakuwa aliyeandaliwa toka mwanzo, anayeonekana ni model mpya aliyeokoa jahazi baada ya model aliyekuwa ameandaliwa kila kitu nguo na malipo kutopokea simu siku ya kushoot na baadaye kusema hataweza tena kushoot video hiyo.

“Siku ya pili ya kushoot hii video ilikua ni birthday ya yule video Queen mpya, kwa hiyo alikuwa na keki yake alinunua, tukaja tukamuomba jamaa atuwekee kwenye fridge tukaenda location akaalika marafiki zake waje kwenye birthday, bahati mbaya tukachelewa location kwahiyo kurudi tukakuta jamaa wamefunga na wameondoka kwahiyo keki imebakia kwenye fridge huku watu wamealikwa lakini hamna keki”-Nikki.

3. Location ya Hotel

Ile sehemu ya hotel iliyotumika kwenye Nje Ya Box ni Kibo Palace Arusha, ambapo wanaonekana wakihudumiwa na mzee mmoja aliyechangamka, meneja wa hotel hiyo alitaka naye abadili mavazi ili naye atokee kwenye video, kitu ambacho Nikki amesema si kawaida.

“tunazoea kwendaga sehemu nyingine unakuta watu wakubwa au wazee hawapendi video lakini cha kushangaza pale Kibo Palace meneja wa ile hotel alikuwa anataka kutokea kwenye video, aling’ang’ania avae acheze kama mhudumu pale Nisher tu ndio alikataa”-Nikki.

4. Box lenye taa walilotumia kwenye video

Box lililotumika kwenye video sehemu ambapo Joh Makini, Nikki na G Nako wameonekana wakiimba limetumia taa za tube lights 48 kutengenezwa.

“halafu siku ya kwanza tulivyoenda, zilikuwa haziwaki zote zilikuwa zinawaka kama 20 hivi, kwahiyo ilibidi lifumuliwe lisukwe upya kwahiyo siku hiyo hatukuweza kushoot tukaja kushoot kesho yake. Kwahiyo ilibidi ile warehouse tukodishe mara mbili kwasababu tulikodisha siku ya kwanza tukafeli kwahiyo ikabidi siku ya pili tuilipie”-Nikki.

5. Ghetto lililotumiwa na Joh Makini na video vixen

Lile ghetto ambalo Joh alitumia na yule mrembo ndimo alipokuwa akilala Nikki wa pili wakati anasoma toka kidato cha kwanza.

“halafu watu wengi wanaoonekana pale ambapo Joh anacheza draft ni watu wa mtaani kwetu yani tumekua nao ni majirani, pia kuna wadogo zangu wawili wapo kwenye ile video”-Nikki

6. Imeweka Record kwa Nisher na Nikki na Joh

Video ya Nje Ya Box ndiyo video ya kwanza kwa Nikki na Joh kufikisha view 20,000 ndani ya siku mbili

Nisher kupitia Instagram aliandika “Another RECORD for me! #NJEYABOX 2 days 20K”. Hadi sasa video hiyo imetazamwa mara 26,641 Youtube.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents