Burudani

Nikki Mbishi adai wasanii wa HipHop hawapewi nafasi ya muziki wao kusikika

Msanii wa Hip Hop nchini, Nikki Mbishi amedai kuwa sababu inayowafanya wasanii wengi wa HipHop wasi ‘shine’ ni kutokana na redio kuwanyima nafasi ya muziki wao kusikika.

nikki-zohan_full

Nikki ameiambia Bongo5 kuwa muziki wao ungekuwa unafanyiwa promo vizuri kwenye redio na TV wange’shine’ kama wasanii wengine.

“Kitu ambacho kipo Hip Hop imekuwa kikwazo kwenye media, hiyo ni fact huwezi kuiepuka, Hip Hop imekuwa kikwazo kwenye media nyingi, muziki wetu ungepata nafasi ya kusikika tungefia mbali zaidi. Huu muziki ambao unaona unafanya vizuri ni kwasababu umepigiwa promo, bila hivyo usingeusikia,” amesema Nikki.

“Sisi hatukiki kwasababu sisi hatutokei kwenye matukio ya ‘fulani anatembea na fulani’, hatupo kwenye matukio yote ya ajabu, sisi muziki wetu ndio unatufanya tuwe hapa. Pia kikwazo kingine hapa Tanzania hakuna matukio ya HipHop ambayo yanaweza kutuonyesha wasanii kama sisi. Muziki wa Hip Hop ndio muziki wenye influence kubwa sana, tunaangalia kwenye show wasanii wa Hip Hop ndio wanafanya vizuri kuliko wasanii wengine lakini hatujajua wao wanawaza nini maybe ni propaganda tu.”

“Hakuna Hip Hop fulani Hip Hop ni ile ile uchanaji ni ule ule, usiseme kila mtu achane kwenye beat kama ya Lil wayne ili uende na wakati, ule ni muziki ambao Lil Wayne kaamua kuwa nao, lakini hajalazimisha watu wote tuimbe kama yeye. Kwahiyo kila mtu ana njia ya mafanikio yake. Mimi nimebuni njia yangu na wengine wabuni njia nyingine ili mradi tufanye muziki mzuri, lakini ujue muziki ni promo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents