Burudani

Nikki Mbishi adai mfumo wa muziki wa kibongo unawanufaisha wasanii wachache

Rapper Nikki Mbishi amedai kuwa ingawa kila msanii anafanya kazi kwa bidii, ni wasanii wachache tu wanaokula kutokana na jasho lao.

916_VZEb2NfGYIVHqJsRsTgtzCevJlXx_b

Nikki amesema wasanii wachache tu ndio wanaonufaika na muziki huku wengi wakikabiliwa na ukata.

“Kazi ni ya wote na shamba ni la wote lakini mavuno ni ya wachache na hiyo iko wazi kwenye industry ya kibongo,” Nikki ameiambia Bongo5. “Kuna kikundi fulani kwenye muziki ambacho wanafanya kazi zao kwaajili ya kuwanufaisha wachache na sisi tunaangalia na sisi tunaendelea na mambo yetu kwa sababu mfumo huu unanufashaisha wachache. Kwahiyo haina haja ya kushindana na watu, kila mtu atengeneze njia zake ajue anafikia wapi. Mafanikio unaweza ukayahesabu kutokana na njia zako wewe na sio kwenye njia zao ambazo wanapita ambazo wanataka na wewe upite. Kwahiyo mafanikio ni kuendelea kuwa hai na kufanya kazi.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents