Burudani

Nicki Minaj azungumzia drama ya Lil Wayne na Birdman, ‘ninawapenda wote wawili’

Nicki Minaj ni miongoni mwa wana familia wa Young Money, na baada ya drama ya boss wake Lil Wayne kutishia kutaka kuondoka Cash Money kwa madai kuwa Birdman anamkwamisha kwa kukataa kutoa album yake , Minaj amezungumzia drama hiyo na kuelezea anachofikiria yeye.

nicki-minaj

“Ninawapenda wote wawili”, alisema Minaj. “Ninaombea kila kitu kiweze kuwa sawa chenyewe kama ambavyo huwa inakuwa kwenye masuala ya familia.”

Aliendelea,

“Mimi ni Young Money, nitakuwa na Wayne kwa chochote. Hivyo ndivyo nilivyo. Lakini Baby [Birdman] amehusika kwa sehemu kubwa katika kuituliza akili yangu. Sijui kama watu wanafahamu, Baby anaweza kukupigia na kukutext siku nzima, ili tu kukufanya ujiskie vizuri, kukufanya ujiskie kuhamasika. Aliwahi kunipigia na kuniambia ‘’Yo, Barbie’, yeye ni kati ya watu wachache ambao bado wananiita Barbie, akasema ‘Yo Barbie, naona matangazo yako kila sehemu, unafanya mambo yako, Barbie, naheshimu hilo’. Huyo ni Baby kwenye simu yangu ananiambia anaheshimu ninavyofanya biashara yangu.”

Nicki hakuishia hapo,

“Unapokuwa juu, huwa kuna lengo moja tu la kuzingatia…Wanatakiwa kutuzingatia sisi, tuko poa. Upendo hushinda vyote. Mi najua hivyo, bila kujali chochote, sisi ni familia, sisi sio marafiki sana wakati wote, lakini ni familia na tunapendana chini ya yote. Ninajua Wayne na Baby wanapendana . Na ninajua watatatua chochote kinachohitaji kutatuliwa.”

Source: BET

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents