Burudani

Nick wa Pili: Maisha uyaonayo kwenye tamthilia au video za muziki ni feki yasikupe stress

Rapper wa kundi la Weusi, Nick wa Pili amewaasa vijana kuacha kuiga maisha ya mastaa mbalimbali wanayoyaona kwenye TV au mitandao ya kijamii kwakuwa si ya kweli na yanapotosha.

Nikki wa Pili_2

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Nick ameandika:

Maisha sasa yametawaliwa na, taarifa potofu ambazo zina aribu, mapenzi, familia , na maadili….taarifa nyingi zinatoka kwa media…(magazeti, tv, radio, blogs, tamthilia, movies, mzk videos)….70% ya taarifa hizi ni za watu maarufu na nyingi niza kutengeneza kwa sababu ya kibiashara ama kulinda hadhi…sio uhalisia hata kidogo wa maisha na hali halisi ya maisha ya watu wengi…sasa upochukuwa taarifa ya maana ya mapenzi, familia, style, mafanikio…katika media ni hatari sana..sasa watu wengi wana unyonge, stress, mapenzi kuvunjika..kufanya mambo ya kijidhalilisha…yote ni kutafuta kuishi kwa maana ya maisha ya kuyasikia na kuyaona kwenye media….kwa kweli stress na unyonge vitaongezeka sana kama kila kijana atatakuwa maisha ya kwenye media na sio ya kwenye mtaa wake na jamii yake..katika uhalisia wa kimaeneo na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents