Burudani

Nick wa Pili: Baada ya miaka 2/3 biashara ya Bodaboda itakuwa haina tija

Msanii wa kampuni ya Weusi, Nick wa Pili amedai kuwa kutokana na kukusanya takwimu mbalimbli kutoka mikoa aliyozunguka amegundua kuwa huenda biasha ya bodaboda ikapotea baada ya miaka kadhaa.

Nikki wa Pili

Akizungumza na wakazi wa Geita leo katika semina ya fursa, Nick amesema kuwa biashara hiyo huenda ikafa mapema kutoka na watanzania wengi kuona ni kimbilio la ajira.

“Katika mikoa yote maeneo tunayoenda bodaboda ni moja wapo kati ya biashara inayoibuka sana,” amesema Nick.

“Lakini inaonekana kwamba kila kijana anataka kununua bodaboda kwahiyo biashara hiyo baada ya miaka 2/3 itakuwa haina tija, yaani itakuwa biashara ambayo haina tija, kwa sababu kila nyumba itakuwa ina bodaboda, utaishia unakuwa na bodaboda labda ubebe ndugu zako.”

“Lakini hiyo inatufundisha nini? Hiyo inatufundisha kwamba vitu vingi tunafanya kwa kufuata mazoea, hatufanyi mambo kimikakati, hatufanyi mambo kwa kuhoji, hatufanyi mambo kwa kujifunza, hatujaribu kujua kwanini sehemu moja inainuka ya nchi na kwanini mikoa mingine inashuka. Kwahiyo mambo kama hayo ndio ya kutafakairi,” alisema Nick.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents