Burudani

Nick Cannon athibitisha kutengana na Mariah Carey, lakini haruhusiwi kuzungumzia talaka

Mume wa Mariah Carey, Nick Cannon amethibitisha kuwa yeye na mwimbaji wa ‘Always Be My Baby’ wametengana, hawaishi pamoja toka mwezi May kama ambavyo ilisemekana.

nick cannon n mariah

“There is trouble in paradise…we have been living in separate houses for a few months,” Alisema Nick Cannon.

Hata hivyo hakuweza kusema chochote zaidi kuhusu talaka na kutengana kwao kutokana na kubanwa na makubaliano waliyosaini.

Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Carey na Cannon walisaini makubaliano ya siri ambayo ni sehemu ya talaka, ambayo hata hivyo yamembana zaidi Cannon.

Katika makubaliano hayo, Cannon haruhusiwi kuzungumzia chochote kuhusu talaka na endapo atakiuka atatozwa faini kubwa, huku Mariah ana haki za kuzungumzia kutengana kwao.

Hata hivyo makubaliano hayo yanamruhusu Nick kuongea kuwa hawaishi pamoja, kitu ambacho tayari amekifanya lakini haruhusiwi kusema chochote kuhusu talaka.

Nick Cannon na Mariah Carey walifunga ndoa mwaka 2008.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents