Habari

Ni kweli sina maeleweno mazuri na mzazi mwenzangu – Barnaba

Barnaba amefunguka kuhusiana na mahusiano yake na mama Steve kwa sasa.

Wiki chache zilizopita muimbaji huyo alidaiwa kuachana na mzazi mwenzake huyo ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, hitmaker huyo wa Lover Boy amesema, “Kwa sasa siko kwenye maelewano mazuri na mama watoto wangu. Sio kwamba tumeachana au tumetengana sitaki kusema hivyo.”

“Siwezi kusema simpendi mwanamke niliyepata nae mtoto [mama Steve],yule ameshakua kama ndugu yangu.Namrespect sana mama Steve ila kila mtu anaendelea na maisha yake na hatutaki kutengeneza picha mbaya kwa mwanetu,” ameongeza.

Wakati huo huo Barnaba amesisitiza kuwa wimbo wake mpya wa ‘Lonely’ ambao ameuachia leo haujamgusa mtu yoyote na wala hausiani na maisha yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents