Michezo

Ni kweli hawa ndio wachezaji anaowafikiria Mourinho kutua nao United?

Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, ambaye anasemekana ataweza kuirithi mikoba ya ukocha ya Louis van Gaal mwisho wa msimu kwa sasa anafanya harakati za kutua na wachezaji watatu kwenye timu hiyo.

ZLATAN_main_2723240a

Rafiki wa karibu wa kocha huyo, Gianluca Di Marzio amesema, “Mourinho ataanza kutafuta achezaji wa nafasi ya beki wa kati, kiungo na mshambuliaji.”

Di Marzio ameendelea kwa kusema kuwa kocha huyo anafikiria kumsajili beki wa Madrid Raphael Varane lakini pia anatamani kuanza kuifundisha United akiwa na Zlatan Ibrahimovic kama mshambuliaji wake kwani anamuona Rooney hataweza kuhimili kasi yake kutokana na majeraha yaliyompata hivi karibuni ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda kidogo.

“Mourinho anafikiria pia kumsajili Stefano Sturaro kwani ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa Juventus,” ameongezea Di Marzio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents