Burudani

Ni kweli Goldie yuko matawi haya?


Aliyekuwa mwakilishi wa Nigeria katika jumba la Big Brother katika shindano la mwaka huu la Big Brother StarGame bibie Goldie Harvey amepiga picha ambazo kama ni kweli basi anaishi matawi ya juu nchini kwao.

Picha hizo ambazo inasemekana amezipiga ndani ya siku mbili zilizopita zinamuonyesha akiwa amefika nyumbani akishuka kwenye gari ya kifahari na fedha nyingi Lambourghini rangi ya njano wakati picha nyingine inamuonyesha akiwa ndani ya nyumba katika chumba chake.

Goldie Harvey akipozi mbele ya gari aina ya Mercedes Ml Class Station Wagon

Well, picha ya tatu na ya mwisho inamuonyesha akiwa amepozi mbele ya gari aina ya Mercedes Benz ML Class rangi ya Blue. Picha hizo zimezua maswali mengi kama ni kweli hizo gari na nyumba anayoonekana ni mali yake, amerithi kwenye familia au zimetokana na jamaa yake ambaye kwa habari za chini ya kapeti inaonekana bado yupo yupo.

Goldie Harvey akipozi ndani ya nyumba

Goldie ambaye pia ni msanii alikuwa katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki kwa takribani wiki nzima iliyopita akianza na jijini Nairobi ambapo alikwenda kwa mwaliko wa kituo cha Televisheni cha Channel O na pia kutumia wasaa huo huo kukutana na Prezzo kabla ya kwenda Uganda ambapo nako alifanya kolabo ya wimbo mmoja na Navio na kisha kumalizia ziara yake Jijini Dar-es-Salaam ambapo amerekodi wimbo na msanii AY ambao umepewa jina la Skibobo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents