Burudani

Ni kweli Alikiba alimfananisha Ruby na mbwa? Ilikuwa ni wikiendi ndefu

Wikiendi iliyomalizika ilikuwa ndefu kwa Ruby. Muimbaji huyo wa ‘Na Yule’ alimrushia shutuma nzito Alikiba kitendo kilichomfanya aoge matusi ya kutosha kutoka kwa mashabiki wa muimbaji huyo ‘Nagharamia.’

12558750_551195738378686_924187961_n

Ruby alidai kuwa Alikiba alimfananisha na ‘mbwa.’

“Well well well kabla ya yote naombeni sana mashabiki zangu, mniwie radhi kwa nnachokiandikia katika ujumbe huu binafsi mimi sijapendezewa kabisa na alichokisema kaka yangu @officialalikiba kwenye kipindi cha @thesporahshow kilichorushwa kupitia @cloudstv kaka yangu alikiba mimi ni mdogo sana kwako si kwa umri wa kimuziki, sikutegemea na sijapendezwa na kauli yako yakunifananisha mimi na MBWA,” aliandika Ruby.

“Mimi ni binaadam na ni mdogo wako kama alivyo @zabibu92kiba sidhani kama ungeweza kumwita huyo mbwa wako zabibu au abdul, mimi sina ukaribu wowote na wewe lakini kama mtu niliyemkuta kwenye industry na uliyenitangulia kuliona jua na mpaka uliponifwata kuniambia una- appreciate kazi yangu nakuniomba nifanye nyimbo na mdogo wako @officialbdukiba na nikakubali yote hayo yalifanikiwa kutokana na love niliyokuwa nayo kwako kama kaka yangu,hujawahi hata siku moja kunitamkia kwamba unambwa wako anaitwa Ruby, kwa sababu mimi na wewe tumesha kutana nakuongea si chini ya mara moja, hujawahi kusema hilo kwangu, ila umekuwa ukiniambia tu naimba vizurii, je ulisahau nini kaka yangu hadi kushindwa kuniambia muhusika wa jina la mbwa wako mpya,mimi nimeona ni kejeli na dharau kubwa na hazisaidii katika maisha zaidi ni kujishushia heshima yako haipendezi kwa mtu kama wewe ambae pia unaangaliwa na watu wengi kama kioo cha jamii,nategemea kuona mfano mzuri kutoka kwako nikiwa kama mdogo wako lakini umenitia giza machoni,”
aliongeza.

“@officialalikiba kakaangu kwakweli nimekwazika sana kwasababu mimi ndo kwanza naanza game naanza kazi ya kuendeleza nchi hii na afrika kwa dunia nzima kwenye upande wasanaa ambao wewe umeshaanza muda ,lakini nimestaajabu unanifananisha na mbwa ,cha ajabu zaidi hata watu wako wa karibu @rehemavisuallab @zabibu92kiba hawaitamki wala kuileta katika jamii kwa usahihi wa mbwa kweli ,Naamini Mungu hamtupi mja wake, chozi la mnyonge haliendi bure, Me namuachia Mungu.”

Post hiyo iliwaamsha mashabiki wa Kiba waliogeuka kuwa nyuki waliochokozwa na kuishambulia post ya Ruby kwa mvua ya matusi.

Alikiba alikiri kosa na kueleza kuwa huenda Ruby alimwelewa vibaya lakini aliona ni vyema akamuomba radhi.

index

Hata hivyo Ruby alirejea na post nyingine;

Asante sana kaka @officialalikiba Msamaha wako nimeupokea na nimekubali japo umeondoa post yako. Utakuwa na sababu zako unazojua mwenyewe. Kama nilivyosema mwanzo issue sio jina la mbwa wako, issue ni huo ‘mfugo’ uliofanywa topic na watu wako wa karibu na kunifanya nianze kuhisi huenda ulikuwa na maana nyingine. Since umepiga simu kwa boss wangu kuomba radhi, mimi sina kinyongo, naomba Mungu huyo mbwa awe anabweka tu ha ha,tufanye tu kazi kaka.”

Kuanzia hapo, kila anachopost muimbaji huyo kimekuwa kikipokelewa na mvua ya matusi. I guess it was a very long week for Ruby.. Oopps.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents