Michezo

Ngumi zamchanganya Shamimu

1_Tamimu_akivishwa_mkanda

Mpiganaji wa ngumi aina ya Boxer ambaye alikuwa akiutetea mkanda wake, Shamimu Award ameibuka na ushindi kwa kumtwanga mpizani wake Ashraf Suleiman, katika Round ya saba, katika kiwanja cha DDC mlimani Cyte.  Katika pambano la uzito wa juu la round kumi, kati ya bingwa wa Afrika mashariki Shamim Award nabingwa wa Afrika Ashraf  Suleiman lilikuwa la nguvu kwani kila mmoja hakutaka kuaibika na kupoteza cheo chake kwa wenzake.


Ilikuwa piga nikupige, angusha nikuangushe, fumua nikufumue lakini kama ilivyokawaida ya mchezo wowote lazima mshindi awe mmoja, na ndiyo sheria ya pambano la ngumi ambalo Shamimu aliibuka kidedea.

Baada ya pambano kama kawaida ya mchezo wa ndundi mshindi alikabidhiwa mkanda, na ndipo baada ya hapo likaibuka tatizo jipya ambalo kwa namna mmoja au nyingine watu hawakutarajia kutokea, ingawa kwa mara chache sana hutokea.

Shamimu baada ya kuchukua ubingwa alianza kupiga kelele na kuongea vitu ambavyo havikueleweka hata kidogo, Kampuni ya Aurola ambayo ndiyo iliyokuwa ikisimamia na kuandaa pambano zima lilijaribu kumweka sawa ilikuona kama kuna tatizo la kumsaidia wamsaidie lakini mambo yakawa tofauti kabisa.

Award alianza kupiga kelele ambazo ziliashiria kuchanyikiwa kidogo, huku akikimbia ovyo na kuwapa tabu walinzi kuweza kumzua, kwani hata wao walihofia usalama wao kwa kipindi hicho.

mpaka naondoka katika uwanja huo, bado walinzi walikuwa wakihaha katika kulisolve tatizo, ambalo limeonekana kuwa balaaaaaaaaaaa.

 

Tamimu_Award_akiingia_ulingoni
(Tamimu akiingia uwanjani, kabla ya kupanda ulingoni)

Tamimu_akijiandaa
(Hapa akijiandaa, akisubiri zamu yake iliapande)

Mku_wa_polisi_wa_kinondoni
(Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni Charles Kinyela naye alikuwepo kama mgeni lasmi (Wa katikati) na aliyeshika makaratasi ni mratibu wa pambano hilo Shomari Kimbau, wakiomboleza kwa dakika kadhaa kwa waliokufa kwa mabomu Gongo la Mboto)

tAMIMU_AKITANGAZWA_MSINDI
(Hapa Shamimu akitangazwa mshindi, baada ya round ya saba kushindwa kuinuka kwa Ashraf Suleiman)

Tamimu_akiwa_nafuraha_ya_ushindi
(hapa akionyesha’Panchi’ zake wakati akisubiri mkanda)

Tamimu_na_meneja_wake_wakishangilia_mkanda
(Sasa Shamimu Award anarudishiwa mkanda wake, ambao ametolea jasho kwa Ashraf Suleiman)

tAMIMU_akishangalia
Shamimu akishangilia ubingwa, kabla ya kupatwa na matatizo, wacheza ngumi na wapenzi wa ngumu wakiwa na wananchi kwa ujumla muombeeni ili aweze kuwa ‘Fit’ na kusaidia mchezo wa ngumi uweze kusonga mbele hapa Tanzania kwetu……. Amen

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents