BurudaniVideos

Ngoma yangu ‘K’ imeongeza idadi ya simu za promota wanaotaka show – Roma

Rapper Roma Mkatoliki amesema ngoma yake ‘K’ yenye mahadhi ya Singeli na aliyofanya na Baghdad imeongeza idadi ya simu anazopigiwa na mapromota kwaajili ya show.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Roma amesema wimbo huo umekuja na neema tafauti na watu wanavyofikiria.

Amedai kuwa mapromota wengi wamekuwa na mawazo wa kufanya naye show zenye majina ya wimbo huo. Na pia amedai kuwa hivi karibuni aliitumbuiza ngoma hiyo jukwaani na watu wakapagawa vibaya.

Kwa upande wa watu wanaoukosoa wimbo huo, Roma amesema aliamua kubadilika kuwaonesha mashabiki kuwa ana uwezo wa kufanya muziki wa aina mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents