Burudani

Ngoma mbili mpya za Roma Mkatoliki zinakuja

Roma Mkatoliki anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa mpigo kabla mwaka haujamalizika. Miongoni mwa ngoma hizi ni pamoja na ile iitwayo One Two, One Two itakayokuwa ikiendana na siku yake ya kuzaliwa.

Roma

Roma ameiambia Bongo5 kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwaridhisha mashabiki wa muziki.

“Project zipo zaidi ya moja ili kufungua mwaka na nguvu mpya, kwa sababu toka mwanzoni mwa mwaka niliwaambia nitatoa nyimbo tatu, nikatoa ya kwanza ambayo ni KKK baada ya hapo zilikuja project za mchangio za gombania goli, tukapiga kolabo na Suma Mnazareti na Moni na Godzilla na baada ya hapo ukimya ukaendelea. From then tunaangalia ni ngoma gani mbili za kumalizia mwaka ambazo anytime zitakuwa hewani. Nazo itakuwa ni zaidi ya nyimbo moja kwa mkupuo. Kuna nyimbo moja inaitwa One Two, One Two yaani Moja Mbili, Moja Mbili hiyo ni tarehe yangu ya kuzaliwa tarehe 12 mwezi 12,” amesema Roma.

Kuhusu video ya wimbo aliofanya na Bob Junior ‘Maumivu’, Roma amesema:

Ni mara ya kwanza kufanya kazi na Bob Junior. kwahiyo unakuta kila mtu yupo busy na mambo yake. Wimbo wa Maumivu haukuwa Roma f/ Bob au Bob f/ Roma, huu ulikuwa wimbo wa wote. Tulipaswa wote tuweke nguvu sawa pamoja lakini tunapishana sana huwa ana show zake mara kwa mara na Roma huwa na show zake mara kwa mara. Kwahiyo mimi ninaweza sema hata ichelewe vipi lazima tutashoot video ya Maumivu na itatoka.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents