Burudani

Ngoma 10 kali ambazo hazikuwahi kupata tuzo

Huu ni msimu mwingine wa tuzo za muziki za Kilimanjaro. Ni muda ambao nyimbo na wasanii waliofanya vizuri hutunzwa! Nimekuandalia orodha ya nyimbo 10 zilizohit sana lakini hazikubahatika kushinda tuzo.

1283-110-music-trophies-12864-p

Mbagala

Ulikuwa wimbo wa taifa kwa wakati ule. Ungesema nini kuhusu Mbagala? Pamoja na kufanya vyema, ngoma hii ya pili iliyompa Diamond nomination ya kwanza ya tuzo za MTV MAMA, ulipita bila kushinda tuzo za KTMA.

Kwa wengi, huu unabaki kuwa moja kati ya nyimbo bora za muda wote kwenye Bongo Flava. Asante Bob Junior kwa zawadi hii.

Sumu ya Penzi

https://www.youtube.com/watch?v=HsvilZ9g0Ds

Kwa mujibu wa Belle 9 wimbo huu ndio wimbo bora wa mapenzi kwenye Bongo Flava kuwahi kufanyika. Hata hivyo huu ni wimbo uliomwanzishia mkosi wa kutowahi kushinda tuzo hizo hadi leo.

Sihitaji Marafiki

https://www.youtube.com/watch?v=iMRtYxpWhuo

Akimshirikisha Mzambia, Yvonne Mwale, mwaka 2012, Fid Q alitengeneza anthem ya hip hop iliyoshindwa kufua dafu kwenye tuzo hizo.
Beat nzuri kutoka kwa J-Ryder wa Tongwe Records iliufanya wimbo huu kuwa ni ni wimbo fulani ambao ungemfanya Ngosha ajikusanyie tuzo kadhaa.

Bado Nipo Nipo

Binamu alileta neno jipya mtaani ni kama ilivyo kawaida yake. Kutoka pale kila mtu ukimuuliza utaoa lini angekujibu bila hofu ‘Bado nipo nipo kwanza’
Hata hivyo wimbo huu haukuongeza tuzo yoyote kwenye kabati la Hamisi.

Rizi One

https://www.youtube.com/watch?v=SPE_mubFbFE

Ongea na Mshua. Ni wimbo fulani mkubwa uliompa heshima Izzo Bizness. Hutakosea ukiuweka wimbo huu miongoni mwa nyimbo bora za Hip Hop ya Bongo za muda wote.

Meseji kali ya hali jinsi ilivyo ngumu mtaani ilikuwa ni idea nzuri kumpa ujumbe ule Rizi One aupeleke kwa mshua wake kule Magogoni ferry.

Rizi One aliufikisha ujumbe? Mimi na wewe hatujui tunachojua ni kwamba kazi hii nzuri haikumwezesha kupata tuzo yoyote.

Sio Mimi (Pombe Yangu)

Jamaa alikuwa zake Bar anapata moja moto, moja baridi. Ghafla akashikwa zake na haja ndogo na kuamua kwenda chooni ambako alibaki mdomo wazi kuona Kademu na Ka-men wakitumia choo kimoja kabla mshangao haujamtoka ile anarudi kwenye meza yake anakuta bia yake imemwagika na kila mtu anasema, ‘Sio Mimi’.

Ni wimbo mkubwa uliomleta Madee na style yake mpya ambayo pia ilimuingizia hela nyingi kuliko style yake ya mwanzo.
Kwa mujibu wake mwenyewe, Madee aliingiza zaidi ya shilingi milioni 150 kwa wimbo huu peke yake japo ulikosa tuzo.

Majanga

https://www.youtube.com/watch?v=5Eqi7iPyVMg

Kutoka kwenye movie mpaka kwenye muziki. Yalikuwa ni mabadiliko ya ghafla mno ambayo kila mtu hakuyategemea kutoka kwa Snura ila alileta kitu kipya kwenye muziki.

Sizungumzii kuhusu viuno vyake, no nazungumzia ukubwa wa huu wimbo ambao hata hivyo umemfanya kuwa ‘one hit wonder’.

Single Boy

https://www.youtube.com/watch?v=-iwnqnbH5N8

Wimbo mwingine mkubwa kutoka kwa Alikiba na humu alimweka ‘Dada Mkuu’, Lady Jaydee kuufanya uwe wimbo mkubwa zaidi kutoka kwa watu wakubwa.

Mwisho wa siku ulipita kama zilivyopita nyimbo nyingine nyingi za Ali K bila kupata tuzo.

Nishike Mkono

Kwa watu wengi huu ulikuwa wimbo bora wa hip hop kwa wakati wake. Jamaa kutoka Kiwalani, Darassa alieleza mambo mengi magumu ambayo yapo kitaani ila mwisho wa siku aliishia kuziona tu tuzo zikienda kwa wengine.

Alisema

https://www.youtube.com/watch?v=13MdmzdNzvk

Stamina ni zao la style ya Fid Q, Like father like son. Wote wamekuwa na bahati mbaya na tuzo hizi ingawa mwaka jana Ngosha aliuvunja mwiko kwa tuzo mbili. Alisema ulikuwa ni wimbo mzuri uliokuwa na kiitikio kizuri kutoka kwa Juma Jux ila haukuongeza tuzo yoyote kwenye sebule ya jamaa huyu wa Mji kasoro bahari.

Makala imeandika na Heri Best
Instagram:Heri Best
Twitter:Mimi_Heri

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents