Burudani

NeyLee kumshirikisha Ali Kiba kwenye wimbo mpya ‘Dunia’

Mshindi wa Serengeti Fiesta Supa Nyota 2012,NeyLee anatarajia kuingia studio ya Mazoo Records kurekodi wimbo wake mpya ‘Dunia’ atakaomshirikisha Ali Kiba.

page

NeyLee amesema kwasasa wanachosubiria ni kuingia studio na kurekodi wimbo huo kwakuwa maandalizi yote yamekamilika.

“Sasa hivi nataka nibadilike niimbe nyimbo za kukimbia kidogo kwasababu muziki ni biashara kwahiyo inahitajika uangalie nini kinahitajika ili ufanye. Kuna nyimbo ambayo nimeiandaa inaitwa ‘Dunia’ ambayo nitamshirikisha Ali Kiba. Watu wangu wasubiri ngoma kali kutoka kwa NeyLee akiwa amemshirikisha Ali Kiba,” muimbaji huyo ameiambia Bongo5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents