Burudani

Neylee aeleza alichokiimba kwenye wimbo mpya ‘Hasara Roho’

Mshindi wa Serengeti Super Nyota 2012 kutoka mkoani Mbeya, Neylee amesema wimbo wake mpya ujao ‘Hasara Roho’ unaelezea changamoto mbalimbali za maisha ya binadamu na jinsi ya kuachana nazo.

10724266_1501143466838859_1551409292_n

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa katika maisha ya binadamu kuna vitu unaweza kukutana navyo na vikakuvunja moyo.

“Hasara Roho ni wimbo ambao kwanza unajieleza katika hali ya kawaida,” amesema. “Hasara Roho ni kama kulipotezea jambo ambalo lilikukwaza, sasa unaamua kuachana nalo kabisa. Sio mimi tu kila binadamu anapitia changamoto, sema tunapambana nazo na kuacha maisha yaende mbele,kwahiyo wimbo utatoka hivi karibuni.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents