Michezo
Newcastel United yawanyatia Benitez na Moyes
Timu ya Newcastle United ipo kwenye harakati za kutafuta kocha mpya ambaye atapokea mikoba ya kocha wao wa sasa Steven McClaren.
Ni miezi nane tu tangu McClaren aanze kuifundisha Newcastle lakini ameonekana kuwa na wakati mgumu ndani ya timu hiyo, kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.
Taarifa za chini ya timu hiyo zinasema kuwa mabosi wa timu hiyo wamependekeza majina ya Rafa Benitez na David Moyes, wakitaka mmoja wao asajiliwe aweze kuiokoa timu hiyo kwenye msimamo wa kushuka daraja huku zikiwa zimebaki mechi tisa tu ligi kumalizika.