Burudani

Nedy Music afunguka aliyopitia kwenye muziki kabla ya kusaini PKP

Msanii Nedy Music amefunguka aliyowahi kuyapitia wakati wa safari yake ya kutafuta mtu wa kumsimamia katika muziki kabla hajakutana na uongozi wa PKP.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5, “Unaweza ukafika sehemu unazungumza na mtu labda akusimamie, kwa baadhi ya wengi unakuta wanakudanganya au wanakujaza tu wenyewe wanasema, unaambiwa fresh tu tutafanya hivi unarudi nyumbani unafurahi unaamini kuwa vitu vitaenda sawa na sasa hivi watu watamjua Nedy Music ni nani lakini inafika mwisho wa siku hakuna kinachofanyika.”

“Nakumbuka kitambo sana kipindi nipo kwa mama Kigamboni nilikuwa naweza kupanda pantoni kuvuka na kuja mjini nahangaika kwenye studio na naombaga zile zamani walikuwa wanasema tafuta lebo katika studio kurekodi bure kwa sababu huna kipato. Niliwahi kuhangaika na kufika Kinondoni kwa sababu nilisikia kuwa ukifika Kinondoni ndio utakutana na wasanii wakubwa,” ameongeza

Hitmaker huyo wa Rudi ameendelea kwa kusema, “Nilipofika Kinondoni kuna studio, Kadriki kipindi hicho ndio anaingia, nakumbuka nilivyofika niliongea naye lakini naogopa sasa natetemeka kwamba nakutanishwa na meneja labda wa studio au producer mkubwa anayemiliki nini nitamwambia kuna vitu niimbe bado sivifahamu.”

“Lakini niliamini nimekuja kutafuta kitu fulani kwahiyo kama sitaonyesha uwezo wangu hakuna ambaye ataweza kujua. Hivyo ni vitu ambavyo nilivipitia huko nyuma. Kuna wakati naingia studio naambiwa hujui au unaambiwa tukikuchukua hapa utatukalia tu, vitu kama hivyo nilikutana navyo lakini niliamini ni changamoto ambayo iliweza kunijenga vema mpaka kutafuta sehemu ambayo haikuwa hata size yangu hatimaye niliweza kukutana na uongozi wa PKP ambapo safari ndio ilianza rasmi.”

Nedy ameongeza kuwa aliwahi kujifunza muziki THT kwa kipindi cha mwaka mmoja kitu ambacho watu wengi wamekuwa hawakifahamu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents