Burudani

Ne-Yo akikubali kipaji cha uchoraji cha Mtanzania huyu, aipost picha yake kwenye Instagram

Chrissy Renny ni kijana mwenye kipaji kisicho cha kawaida – anachora picha kwa kutumia kalamu ya wino ambayo ukiilinganisha na picha original, unaweza kudhani aliyochora ni photocopy.

11355779_1758489101044312_1544457717_n
Picha ya Ne-Yo iliyochorwa kwa mkono kutumia kalamu ya wino

Cha kufurahisha zaidi, Chrissy ni Mtanzania na sasa jina lake limefika Marekani – thanks kwa shavu alilopewa na Ne-Yo.

Chrissy ambaye huchora picha za mastaa anaowapenda na kuziweka kwenye akaunti yake ya Instagram, alimsurprise Ne-Yo aliyekuwa nchini Afrika Kusini wiki iliyopita kwenye MTV MAMA, kwa kuchora picha yake.

“A pen drawing of Ne-yo can’t wait for his performance on #mtvmama today 18 july, #nonfiction2015 #neyonation #neyo please tag him too @neyo, aliandika Chrissy kwenye picha hiyo.

Ne-Yo ameipenda picha hiyo na hakusika kuipost kwenye akaunti yake yenye followers milioni moja na kuandika, “This is dope! Shout out to @chrissrenny #NEYONATION #Art #NONFICTION2015.”

Tangu aanze kuchora picha za mastaa mbalimbali, Ne-Yo ndio msanii wa kwanza wa Marekani aliyeiweka picha hiyo kwenye akaunti yake na ndio maana Chrissy amekipokea kitendo hicho kwa furaha kubwa.

“Am shocked thank you neyo for the appreciation and thanks to everyone for the tags you guys are so dope @neyo @evey1,” aliandika Chriss.

Tayari Chrissy amepata mashabiki duniani kote.

“@neyo liked and shared @chrissrenny …that’s how I came here..love your work. Greetz from The Netherlands,” ameandika msichana mmoja kutoka Uholanzi.

Chini ni baadhi ya picha za mastaa alizochora Chrissy.

11417419_1877332142491841_1982906024_n
Msanii wa tamthilia ya Empire, Taraji P Henson

11005027_1377174452590106_586656760_n
Linah

11023167_1436397596653282_743025334_n
Rihanna

10731708_510198685750375_2126167805_n
Chris Brown

10808784_1510668029204685_98118448_n
Rihanna

10843887_404450439713346_2027170782_n
11195668_1609196952696806_328265993_n
Profesa Jay
11085069_811972012229134_1560772809_n
Ciara
10895413_1602121310016356_1633677158_n
Yemi Alade

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents