Burudani

Ndoa ya Jay Z na Beyonce itavunjika ‘soon’, vyanzo vya karibu vyasema

Ndoa ya Jay Z na Beyonce inaweza kufikia tamati siku si nyingi zijazo. Pamoja na hivi karibuni mastaa hao kujionesha mbele za watu kuwa bado wanapendana, kuna tetesi zinavuma kuwa wanaelekea kuachana rasmi.

beyonce-and-jay-z11

Kwa mujibu wa ripoti iliyoandikwa na New York Post, Hov na Bey wanapanga kuachana watakapomaliza ziara yao ya On The Run. ‘Wanajaribu namna ya kuachana bila kupeana talaka,’ chanzo kimoja kililiambia New York Post. ‘Hii ni ziara kubwa na wameshalipwa karibu fedha zote kutoka kwa mapromota.’

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mastaa hao wameacha kuchukuliana kama mume na mke na hawavai tena pete zao za ndoa.

Inadaiwa kuwa Jay na Bey wamekuwa na matatizo kwenye ndoa yao kwa miaka mingi tangu mtoto wao Blue Ivy alipozaliwa mwaka 2012. ‘Walidhani mtoto anaweza kusababisha mambo yanyooke. Walifanya kosa kubwa kudhani kuwa mtoto anaweza kuuwasha tena moto wa zamani, lakini haikuwa hivyo.’

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents