Burudani

‘Ndoa inafuata’ adai Nuh Mziwanda baada ya kumvisha pete ya uchumba Shilole

Nuh Mziwanda na Shilole ni wachumba halali. Nuh alimvisha Shilole pete ya uchumba weekend hii wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa kibao.

Nuh  akiibusu pete ya uchumba aliyomvalisha Shilole

Nuh ameiambia Bongo5 kuwa ndoa ni hatua inayofuata muda si mrefu.

“Kila siku naupdate vitu vipya katika maisha yake, nimechora tattoo ya kwanza Shishi baby, nikaja tena kwa kumuonyesha simchoki nikachora uso wake,” amesema msanii huyo. ” Imekuja tena nimemvalisha pete ya uchumba yaani najitahidi sana kuonyesha jinsi gani nampenda. Yaani anajiuliza ‘mwanaume wangu mimi ananichora hii’ inamtia moyo na kumpa matumaini makubwa sana.”

“Kumvalisha pete ya uchumba ni kama baraka hata hapa ninavyoongea Mungu ananisikia. Sasa anytime ninaweza nikamuoa, kinachofuata ni kumuoa kwahiyo tuombe uzima tu,” aliongeza.

Hivi karibuni Nuh aliachia single yake mpya ‘Zima Taa’.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents