Habari

Nchakalih, Hermy B na Miss E.Africa 2012 kesho kuichambua albam ya Jay-Z ‘MCHG’ kwenye The Switch ya Times FM

Aliyekuwa mtangazaji wa Clouds FM, Reuben Ndege aka Nchakalih, producer wa B’Hits Music Group Hermes Tyrol Lyimo aka Hermy B na Miss East Africa 2012, Jocelyne Kimaro kesho wanatarajiwa kuichambua albam mpya ya Jay-Z ‘Magna Carta Holy Grail’ kwenye kipindi cha The Switch cha Times FM 100.5.

JayZ_MagnaCartaHolyGrail_608x608

The Switch huruka kuanzia saa 6 mchana hadi saa 10 jioni.

Akiongea na Bongo5, mmoja wa watangazaji wa show huyo Raheem Da Prince amesema wamemchukua Jocelyne kwenye panel ya wachambuzi wa albam hiyo kwakuwa anaijua hip hop kwa undani.

immm
Jocelyne

“Anaijua hip hop kuliko unavyofikiria wewe,” amesema Raheem. “Tumeweza kuweka kama equality, hatuwezi kuweka wanaume peke yake halafu hakuna mwakilishi wa wanawake kwasababu tunaamini mtaani kuna watu wanaopenda hip hop na kuijua vilevile.”

“Tumemwalika Miss East Africa kwasababu yeye ni public figure na pia anaijua hip hop na anaipenda.”

“Yaani sasa hivi kila mmoja yupo chimbo, anaisikiliza ngoma hadi ngoma, historia ya Jay-Z anayoijua yeye anaongeza na madini kwahiyo kesho ikifika ngoma moja hadi ya mwisho tunazichambua.”

Msikilize zaidi Raheem hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents