Burudani

Nay wa Mitego: Nilikaa miaka 5 bila ya kuongea na mama yangu mzazi

Nay wa Mitego amefunguka kuwa aliwahi kukaa miaka mitano bila ya kuongea na mama yake mzazi.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Sijiwezi’ amekiambia kipindi cha Planet Bongo Cha EA Radio Ijumaa hii kuwa kitendo hicho kilitokana na mazingira ya mtaani aliyokuwa anaishi lakini kwa sasa anaishi pamoja na mama yake na wako poa kabisa.

“Mimi na mama mzazi tuko poa sana na nina kaa naye this time. Ni kweli kabisa tumekaa miaka mitano bila kuzungumza jambo lolote lile, ila ni mazingira ya maisha ya mtaa niliyokuwa naishi lakini mpaka muda huu tunaongea mimi naishi na mama yangu nyumbani kwangu, hivyo niko naye nyumbani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents