Burudani

Nay wa Mitego kutoa video mbili tofauti za Akadumba

Nay wa Mitego amesema wimbo wake mpya wa Akadumba aliouachia hivi karibuni utakuwa na video mbili tofauti.

10808438_860003930710934_545541262_n
Nay wa Mitego

Nay amesema kutokana na maudhui ya video, atafanya video mbili ili kutoa ladha mbili tofauti kwa mashabiki wa muziki wake.

“Nafikiri nahitaji kuwa na video mbili za huu wimbo halafu baadaye tutajua nini cha kufanya. This time nipo mbioni kuandaa maandalizi mazuri kwaajili ya video na panapo majaliwa nitasema ninaenda kushoot sehemu. Sitaki kusema ni wapi lakini panapo majaliwa kila kitu kitajulikana Sasa watu wapo kwenye mazoezi kwaajili ya kukamilisha kufanya video ikawa video inayoendana na wimbo,” Nay ameiambia Bongo5.

Kuhusu maana ya wimbo huo, Nay amesema:

“Akadumba wimbo kabisa nimemwimbia mwanamke, ni kama mwanamke na pia ni style ya mwanamke ya kucheza ambayo wanawake wengi wanaitumia sana. Pia wanaume wanaweza kuicheza, yaani ni uchezaji fulani hivi ninaweza kusema wakitanzania au wakiafrika ambayo haswa wanaoweza kuicheza zaidi ni wanawake kwa viungo vyao. Pia wanaume wanaweza. Akadumba ni neno ambalo tu lilikuja wakati tunatafuta pa kuanzia ili tupate wimbo, kwahiyo nia yangu ilikuwa ni kutafuta nyimbo nzuri ya kuchezeka. Unajua watu wa Nigeria wamechukua nafasi kubwa sana kwenye muziki wetu ndio maana nikaona na mimi nitengeneze kitu fulani ambacho kitakuwa cha kuvutia.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents