Burudani

Nay wa Mitego asema hawezi kuacha kufanya muziki anaofanya kwa kuogopa nyimbo zake kufungiwa

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego licha ya kuwa kwenye kikao kizito na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) baada ya kufungiwa kwa wimbo wake ‘Pale Kati’ kwa kigezo cha maadali, rapper huyo amesema bado ataendelea na muziki wa aina hiyo kwa kuwa mashabiki wake ndiyo mabosi wa muziki wake.
Nay wa Mitego

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay amesema kila msanii ana njia yake ambayo ameitafuta ili aweze kueleweka na mashabiki wake ambapo akidai ni ngumu kumbadilisha msanii wa namna hiyo ili afanye kitu tofauti.

“Unajua mimi tayari namashabiki wangu ambao wanapenda muziki wangu toka naanza mpaka sasa, na tayari wameshajua wanafuata nini katika muziki wangu na siwezi kuwapoteza kwa sababu hao ndio mabosi wangu, sio BASATA,” alisema Nay

Aliongeza, “BASATA hawawezi nipangia nifanye muziki wa aina gani, itakuwa ni ngumu sana. Kila msanii ana muziki wake na ana style yake tukisema wote tuimbe kitu kimoja basi tutakuwa tuaimba kwaya. Kila mmoja anatumia ubufifu katika muziki wake ili kuwashawishi mashabiki wapende muziki, na nikwambia kitu mashabiki wa Nay niwa Nay tu, wanampenda Nay kutokana na aina ya muziki ninaoufanya,”

Pia rapper huyo amesema baada ya kikao chake na BASATA kumalizika Jumanne hii, atatoa tamko la nini kimejadiliwa na maazimio yaliyotewa katika kikao hicho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents