Burudani

Nay Lee akanusha tetesi za kuwa mjamzito

Msanii aliyezaliwa kutoka kwenye shindano la Serengeti Super Nyota, Nay Lee amekanusha tetesi zilizopo kwamba ni mjamzito.

Nay Lee alikuwepo kutoa burudani nyumbani

Nay Lee ameiambia Bongo5 kuwa tetesi hizo zinamshangaza.

“Unajua hata mie ninashangaa kila mtu ananimbia ‘Nay Lee mjamzito’ nabaki nashngaa tu,” amesema. “Kama unavyoniona mwenyewe hapa sina ujauzito hizo ni habari ambazo sio za ukweli maana hapa mlipo kila mtu ananishangaa nilivyonenepa, nahisi labda ndio maana wanasema nina ujauzito. Lakini sina, na kwa sasa hivi bado aisee kubeba ujauzito. Najipanga maisha kwanza,” ameongeza.

Kuhusu wimbo mpya, msanii huyo amesema hivi karibu ataachia wimbo uitwao ‘Hasara Roho’.

“Unajua sio kama nipo kimya ila najipanga nadhani sio muda mrefu sana nitatoa wimbo wangu mpya unaitwa “Hasara Roho.” Wimbo nimefanya na producer Zest. Mashabiki wangu wakae tayari kwa ngoma hiyo na pia mara nyingi nimekuwa nakuja Mbeya kwakuwa huku ndo home unajua. Halafu pia huku nima biashara zangu kwahiyo inabidi mara nyingi niwe nakuja kuangalia zinaendeleaje ila bado naishi Dar.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents