Burudani

Nay adai hana taarifa rasmi ya kufungiwa kwa wimbo wake ‘Shika Adabu Yako’

Nay wa Mitego baada ya kuoana taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) imeufungia wimbo wake ‘Shika Adabu Yako’, amedai bado anasubiria taarifa rasmi.
12543311_165915390449197_1955172136_n

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Nay wa Mitego amedai yeye ataendelea na ratiba yake pamoja na kufanya maandalizi ya video.

“Kusema ukweli BASATA hawajui kazi zao. Mimi nashindwa kuelewa sababu ya kuufungia wimbo wangu, hauna tusi lolote zaidi ya kusema ukweli,” alisema Nay.

“Pia kuwachana BASATA ni haki yao kwa sababu hawajui kazi zao, kazi kufungia nyimbo za wasanii. Kwanza mimi sijapata taarifa rasmi ya kufungiwa, pili bado nipo kwenye mpango wa kuchoot video Jumatatu.,” aliongeza Nay

Taarifa ta BASATA inadai wimbo wa Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’ ni wimbo ambao haufai kusikilizwa katika jamii kutokana na kukiuka maadili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents