Burudani

Navy Kenzo waeleza watakavyouza album yao ‘Above In A Minute’

Kundi la Navy Kenzo limesema kuwa album yao ya kwanza iitwayo ‘Above In A Minute’ tayari imekamilika na wanatarajia kuitoa mwanzoni mwa mwaka ujao 2015.

navy2

Wakizungumza kupitia XXL ya Clouds FM, waimbaji wa kundi hilo Aika na Nahreel wamesema kuwa, watauza album yao katika mfumo wa Cd pamoja na online, lakini utaratibu utakaotumika utakuwa ni wa kuweka oda pekee.

“Ila itakuwa ni oda tu, hata kama ni online unafanya oda tu ukishalipia siku ikitoka unapewa ya kwako baada ya hapo itakuwa ni ngumu sana kuuza.” Alisema Aika.

Wameongeza kuwa album hiyo itakuwa na jumla ya nyimbo nane, na wamewashirikisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Japo hawakupenda kutaja wasanii wote kwa sasa lakini wachache ambao wameshirikishwa ni kundi la R2bees la Ghana, na kuna uwezekano wakamshirikisha Patoranking wa Nigeria ambaye yupo Tanzania kwa sasa. Kwa Tanzania ni Weusi, Vee Money na Young Dee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents