Burudani

Nature aapa kutoweka wazi miradi yake, ni baada ya idea ya ndala kuchukuliwa

Msanii mkongwe wa muziki kutoka TMK, Juma Nature amesema baada ya kuibiwa idea yake ya biashara ya ndala amejifunza kutoweka wazi miradi yake iliyopo kwenye ‘pipeline’.

Juma-Nature

Nature ameiambia Bongo5 kuwa amekoma kutangaza miradi yake hadi pale itakapokuwa imekamilika.

“Watu wanakuwa matajiri kwa idea za kwangu mimi, sasa hivi siwezi kuzinadi kazi zangu kwa sababu zinapotea, lakini raia hawawezi jua, kama itakuwa nimeshamaliza kila kitu nimaweza tangaza ila kama bado siwezi, kama idea yangu ya ndala ilivyochukuliwa na yule dogo, mimi siwezi kwenda kwenye media na kutangaza nimeibiwa idea nitakuwa naonekana mjinga, kwahiyo mimi nimejifunza sasa hivi sitangazi kitu mpaka nihakikishe kimetoka tayari,” amesema rapper huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents