Burudani

Natamani kuirudia ‘Kamanda’ ya Daz Nundaz au ‘Mkasa wa Boss’ ya Ferooz – Tunda Man

Msanii wa muziki Tunda Man ameweka wazi nia yake ya kutaka kurudia wimbo wa ‘Kamanda’ wa Daz Nundaz au ‘Mkasa wa Boss’ wa Ferooz kutokana na nyimbo hizo kubeba ujumbe mzito.

Tundaman

Tunda ameiambia Leo Tena ya Clouds Fm, kuwa alijaribu kubadilisha kisa cha wimbo wa Feooz ila akashindwa na kuamua kujipanga na kuuimba kisasa zaidi.

“Mimi sisemei mapungufu kuna ngoma nimezizimia kwa sababu kabla mimi sijaanza kuimba, nilikuwa namsiliza sana Ferooz , kwahiyo kuna ngoma mbili ambazo yani natamani leo, kesho nizirudie, kati ya Kamanda au Mkasa wa Boss. Kwa ile msg mpaka sasa hivi haijaimbwa kabisa, nilikuwa nataka nichukue melody halafu nitafute kisa kingine lakini nishatafuta kisa naona sikipati, naona kama kisa yeye kashakimaliza, nahisi nikiirudia ileile kwa sababu yeye alifanya zamani kidogo, mimi nikiimba nitakuwa nimeiimba kisasa zaidi,” alisema Tunda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents