Burudani

Nataka kumwandikia Alikiba wimbo bure – asema mwandishi wa ‘Basi Nenda’ ya Mo Music

Mtayarishaji wa muziki na mtunzi wa nyimbo wa Mwanza, Lollipop amesema baada ya kutunga nyimbo kama ‘Basi Nenda’ ya Mo Music na ‘Siachani Nawe’ ya Barakah Da Prince na nyingine, amedai kwa sasa anatamani kufanya kazi na Ali Kiba hata ikiwa bila malipo.

Lollipop

Akizungumza na kituo cha redio cha Kitulo FM Kilichopo wilayani Makete, Njombe, Lollipop alisema kila wimbo anaoandaa kwa sasa unagharimu shilingi milioni tano ila kwa Alikiba anatamani afanye naye kazi bure.

“Yaani katika wasanii ambayo nawafeel kufanya nao kazi ni Alikiba hata bure,” alisema. “Alikiba namwelewa sana na by the way nafikiri nitafanya naye kazi fulani. Nakubali sana uwezo wake ana sauti, anaelewa anachokifanya so honestly natamani sana kufanya naye kazi Kiba kuliko msanii yoyote Afrika. Sijawahi hata ku-meet na Alikiba na hatujawai hata kupata muda wa kukaa na kudiscuss lakini hii ni kutokanana na muda. Lakini muda ukifika nitakutana naye na kulizungumzia suala hili,” alisema Lollipop.

Pia Lollipop alisema anawashukuru watanzania kwa kuupokea vizuri wimbo wa Barakah Da Prince ambapo umempa interview nyingi kutokana na uzuri wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents