Burudani

Nash MC ataja 5 bora ya ‘marapa’ wake, yupo Khalid Chokoraa na wengine

Rapa Nash MC amefunguka kwa kuwataja wasanii wa rap ambao anawakubali ikiwa ni siku chache baada ya Nay wa Mitego pamoja na Young Killer kutoa top 5 zao za marapa bora kwa upande wao.

Nash amekuwa tofauti na wengine kwa kutomtaja msanii hata mmoja wa hip hop na kusema kuwa aliyekuwa star wa twanga Pepeta, Ferguson ndiye mfalme wa marapa Tanzania.

Nash MC amesema hayo kupitia mtandao wake wa Facebook na kusema kuwa anaomba orodha yake hiyo ya wasanii watano anaowakubali iheshimike.

“Naona siku hizi kila mmoja anataja Marapa wake bora anaowakubali. Sina budi na mimi niwatajie orodha ya wakali wangu hao watano. Nao ni
1. Khalid Chokoraa
2. Totoo Ze Bingwa
3. Msafiri Diouf
4. Canal Top
5. Khalidjo Kitokororo Kuku

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents