Burudani

Nape adai wizara ya habari itaanzisha tuzo za blog mwakani

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema kuanzia mwakani wizara yake itaanzisha tuzo mahsusi kwaajili ya blog za Tanzania.

waziri-wa-habari-utamaduni-sanaa-na-michezo-mhe-nape-moses-nnauye-katikati-akizungumza-na-wanachana-wa-tanzania-bloggers-network-tbn
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akizungumza na wanachana wa Tanzania Bloggers Network, TBN

 

Akizungumza wakati akifunga mkutano mkuu na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini, TBN jijini Dar es Salaam Jumanne hii, Nape amesema kwa kazi kubwa ambayo blog zimekuwa zikiifanya katika kuhabarisha umma, ni muda wa kuanza kuwatuza wale wanaofanya vizuri.

Amesema alipata wazo la kuja na tuzo za aina hiyo wakati akisafiri kwenye ndege na kuona jarida linaloelezea tuzo za blog za Kenya na kuona kuwa kuna ulazima wa Tanzania pia kuwa na tuzo hizo.

Nape amedai kuwa lengo la tuzo hizo zitakazotolewa mwanzoni mwa mwaka ujao, zitakuwa ni kwaajili ya kuzisaidia blog kuweza kuwa na ‘specialization’ katika maudhui mbalimbali.

Amesema tayari ameshaanza kuzungumza na makampuni na taasisi mbalimbali kwaajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi wanapewa zawadi kubwa ili kuwahamasisha zaidi. Ameahidi kuwa tuzo hizo zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi na kwamba makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents