Burudani

Naomba Shetta usinirudishe enzi za Mr Nice – Dudu Baya

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Dudu Baya amemtaka Shetta kuacha kutumia jina la ‘Mamba’ kwani hiyo ni ‘aka’ yake ambayo amekuwa akiitumia kwa miaka mingi.
Dudu Baya na Mr Nice akiwa wamepozi

Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya alisema anaomba Shetta aache mara moja kutumia jina hilo ili yasije yakatokea kama ya Mr Nice.

“Shetta ni kama mdogo wangu sitaki ugomvi nae, asinirudishe enzi za Mr Nice,” alisema

“Mbona majina yapo mengi kwanini atumie jina langu (Mamba). Naomba afikishiwe huu ujumbe, nimemtafuta kwenye simu hapatikani,” alisema Dudu Baya.

Dudu Baya amedai ameona mara kadhaa msanii huyo anatumia jina lake bila kuongea nae.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents