Awards

Nani Kung’ara Kilimanjaro Tanzania Music Awards leo?? [Video+Photos]


Kile kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za muziki, Tanzania Kilimanjaro Music Awards, kinafikia tamati katika sherehe itakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani Conference Hall usiku wa leo.

Kwa upande wa maandalizi safari hii Meneja Chapa wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, amefanya kazi ya ziada kuhakikisha kwamba watazamaji watapata burudani ya kipekee huko ukumbi ukizidi kushine! Kwa kweli Kilimanjaro Tanzania Music Awards zimefika viwango vya kimataifa, angalieni sneak peek video na picha hapa chini:
[youtube]http://www.youtube.com/watch?v=AecGbjb-tVA[/youtube]
Kinyang’anyiro hicho ambacho kilianza takriban miezi mitatu iliyopita kilizinduliwa kwa sherehe kali, baada ya hapo kamati ya tuzo ilichagua wana akademi wapatao 50 ambao waliingia kambini siku 2 kwa ajili ya kufanya mchujo wa wasanii ambao walitakiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Msanii Nasib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz anaongoza kinyang’anyiro hicho akiwa anawania tuzo 7 akifuatiwa na msanii Ali Kiba ambaye anamfuatia kwa karibu huku akiwania tuzo 5.

Swali lilopo kwenye vichwa vya watu ni je msanii Diamond ataweza vunja rekodi iliyowekwa na msanii 20% aliposhinda tuzo 5 mwaka jana na pia msanii huyo ataweza kumbwaga msanii mwenzake Ali Kiba??

Tusubiri kesho na tuone nini kitatokea Bongo5 itakuwepo ndani ya mjengo kukupa yale yote yatakayojiri.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents