Habari

Namna ya kuweka mlingano sawa wa kazi na maisha mengine

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia, uchumi kukua na kila mmoja anajaribu kufanya kazi ili aweze kufanikiwa kibiashara na kitaaluma. Hakuna tatizo katika kufanya kazi sana lakini kulemewa na kazi nyingi hilo ni tatizo. Siku hizi wataalam wengi katika nyanja mbalimbali wamekuwa wakifanya kazi sana na kusahau maisha mengine yanakwendaje. Ni katika jitihada zao za kujulikana kazini kama mfanyakazi bora, au ili upandishe cheo na nyongeza ya vitu mbalimbali.

Man-Woman-working-from-home

Hivyo wengi wamekuwa wakitumia kutengeneza mikataba ya kazi mbalimbali za kiofisi, vikao, semina na mambo mengi waliyojiwekea kwa ajili yao wenyewe na biashara zao. Kila mtu anajitahidi familia yake iwe na maisha mazuri na kwa huyo mfanyakazi kuhakikisha kazi yake inaendelea kuwepo.

Kama mfanyakazi unahitaji kujifunza namna ya kuishi maisha ya kawaida nje ya kazi. Haimaanishi kama unataka kuwa mtu aliyefanikiwa katika taaluma basi usahau maisha ya kawaida kama muda wako wa kupumzika, kuwa na familia yako, michezo na vitu vingine kama hivyo. Kama unahitaji kuwa na furaha, bila msongo wa mawazo unahitaji tu mlinganyo sahihi wa maisha na kazi.

Inakubidi ujue malengo yako, namna bora ya kutawala muda wako, hivyo shauku yako ya kufikia malengo fulani kimaisha inabidi ijengwe katika mtizamo sahihi bila kuharibu vitu vingine katika maisha yako. Jaribu vitu vifuatavyo kupunguza mrundikano wa kazi, na upate muda wa kufanya vitu vingine;

1. Yatizame kwa upya malengo yako

Kila mtu ana malengo fulani, katika kazi kuna watu wanataka kupata mshahara zaidi, wengine ziada inayotokana na kufanya kazi vizuri zaidi ya malengo yaliyowekwa kazini. Jambo la msingi limekuwa kupata hela , hela zaidi ikiwezekana na kupandishwa ngazi au cheo. Kama ndo sababu ya wewe kutumia muda mwingi kazini, inawezekana unakoelekea si kuzuri, kama unawekeza muda mwingi katika kazi au taaluma yako bila malengo mazuri utafikia eneo utashindwa na kutingwa na kazi nyingi.

2. Kuifanya taaluma yako kama rafiki

Unapochagua biashara au taaluma ni kwasababu unaujuzi wa kazi hiyo na unapenda kufanya kazi hiyo. Inaonekana ni jambo la kizamani lakini wakati wote unatakiwa kukumbuka kwamba unapofanya kitu unachokipenda huwezi kuhisi kama ni kazi.

Sababu ya wafanyakazi wengi kuchukia kazi ni kuichukulia kazi kama adui au kutoipenda na kufanya tu kwasababu ya mshahara. Watu wa aina hii huwa hawaifurahii kazi hata kidogo muda wote hulalamika, maisha yao husongwa na kuchoka vilevile huchukia siku za kufanya kazi. Jaribu kutafuta namna utakavyoipenda kazi yako na ufanye ugunduzi wa vitu vipya katika kazi yako. Furahia unachokifanya na hutachoka kufanya hiyo kazi tena.

3. Usiruhusu kazi kuamua maisha na namna unavyopaswa kuishi.

Watu wengine wanashindwa kushirikiana na jamii kwa kuangalia kazi livyo au ratiba ya kazi, hivyo wakati mwingine hawaendi harusini, misibani hata kupumzika na familia zao na hata kushindwa kuhudhuria ibada za dini zao kwa sababu ya kazi wanazofanya. Kama mtaalamu na kazi uliyonayo unaijua vizuri weka mipaka kati ya maisha ya kawaida na kazi yako kazi yako haitakuwepo milele ila watu na uhusiano na watu wa jamii inayokuzunguka ni wa maisha yako yote. familia na marafiki bado wanakuhutaji na wanahitaji muda wako.

4. Heshimu muda wako binafsi

Heshimu muda wako binafsi kama unavyohesimu muda wa wateja wako na kazi yako. Kama ukiweza kuweka muda wako na kwa ajili ya familia yako, usibebe  kazi za ofisini kwenda nazo nyumbani. Jipe muda mzuri wa kulala na kupumzika ili uweze kuwa na mwelekeo na nguvu za kutosha kufanya kile unachotakiwa kufanya siku inayofuatia.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents